AFRIKA KUSINI-ANC-SIASA

Kiongozi mpya wa ANC kutangazwa baada ya mkutano wa Jumapili

Hajajulikana atakaemrithi Jacob Zuma, mkutano wa Jumapili Desemba 17 ndio utaamua.
Hajajulikana atakaemrithi Jacob Zuma, mkutano wa Jumapili Desemba 17 ndio utaamua. PHILL MAGAKOE / AFP

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC, kinatarajiwa kumtangaza kiongozi mpya wa chama hicho siku ya Jumapili. rais wa Afrika Kusini ambaye ndiye kiongozi wa sasa wa chama cha ANC anaendelea kukabiliwa na kashfa ya ufisadi.

Matangazo ya kibiashara

Ushindani ni kati ya Naibu rais Cyril Ramaphosa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika  Nkosazana Dlamini-Zuma .

Mshindi atakuwa mgombea urais mwaka 2019 na anatarajiwa kuleta umoja ndani ya chama hicho.

Mapema mwezi Novemba Makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa aliwambia wafuasi wake kuwa uongozi mbaya umeigharimu ANC na uchumi wa nchi hiyo. Aliwataka wafuasi wake kubadilisha hali hiyo katika uchaguzi wa chama.

Hayo yanajri wakati ambapo rais wa Afrika Kusini Jacob zuma anaendelea kukabiliwa na shutma za ufisadi.

Naibu rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anaelekea kupata uungwaji mkono mkubwa kuelekea mkutano Mkuu wa chama cha ANC, kumpata kiongozi mpya.

Ramaphoza alizaliwa Novemba 17, 1952.