LIBERIA-UCHAGUZI-SIASA

Waliberia waendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi

Zoezi la kuhesabu kura lilianza Jumanne usiku Desemba 26, Liberia.
Zoezi la kuhesabu kura lilianza Jumanne usiku Desemba 26, Liberia. REUTERS/Thierry Gouegnon

Wananchi wa Liberia wanaendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi wa duru ya pili uliofanyika jana Jumanne Desemba 26 kati ya nyota wa zamani wa mpira wa miguu George Weah na Makamu wa Rais Joseph Boakai, uchaguzi ambao waangalizi kutoka nchi mbalimbali walipongeza

Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kuhesabu kura ambalo lilianza siku ya Jumanne usiku,kwa jumla ya wapiga kura milioni 2.1, linatazamiwa kuendelea katika siku zijazo mpaka atakapotangazwa mshindi.

Mshindi atamrithi Ellen Johnson Sirleaf, mwanamke pekee aliyechaguliwa rais katika Afrika na ambaye alipata Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2011. Rais Ellen Johson Sirleaf amemaliza muda wake wa kuhudumu kakama rais wa Liberia. Anatazamiwa kukabidhi madaraka kwa mrithi wake mnamo Januari 22. rais mpya wa nchi hiyo atahudumu kwa kipindi cha miaka sita.

Liberia ilikua haijashuhudia zoezi la kukabidhiana madaraka kupitia mfumo wa kidemokrasia tangu 1944, "kwa sasa jambo hilo limewekzekana na ni muhimu kwa taifa hili la Afrika Magharibi. Ikiwa Liberia imefanikiwa mfumo huo, ni ushindi kwake, vile vile ni ushindi kwa Afrika Magharibi na Afrika kwa ujumla. ", rais wa zamani wa Nigeria, Goodluck Jonathan, kiongozi mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa National Democratic Institute (NDI), taasisi ambayo makao yake makuu yanapatikana nchini Marekani.

Liberia ni nchi inayozungumza Kiingereza katika Afrika Magharibi, ambayo ilikumbwa kwa kipindi cha miaka kumi na nne ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kutisha - watu 250,000 waliuawa kati ya mwaka 1989 na 2003 - na kisha kwa wengine walipoteza maisha baada ya nchi hiyo kukumbwa na ugonjwa wa Ebola, lakini kwa sasa Liberia imeanza kujidhatiti baada ya ugonjwa huo kutokomezwa.