DRC-USALAMA-SIASA

Serikali ya DRC yapongeza vikosi vya usalama kwa kuzima maandamo

Msemaji wa serikali ya DRC, Lambert Mende, akizungumza na waandishi wa habari, Kinshasa.
Msemaji wa serikali ya DRC, Lambert Mende, akizungumza na waandishi wa habari, Kinshasa. FEDERICO SCOPPA / AFP

Viongozi wa serikali ya DRCongo walipongeza vikosi vya usalama nchini humo namna vilivyodhibiti maandamano ya waumini wa kanisa katoliki wanaompinga rais Joseph Kabila ambapo watu 12 wanadaiwa kupoteza maisha, kwa mujibu wa waandaaji wa maandamano hayo.

Matangazo ya kibiashara

Serikali kupitia msemaji wake Lambert Mende, ilisema polisi imetumia uweledi kote nchini katika kuwadhibiti watu ambao nia yao ilikuwa ni kuanzisha vurugu hadi kuiangusha serikali iliopo.

Jana Jumatano, Kadinali Laurent Mosengwo alivituhumu vikosi vya usalama kwa kutumia nguvu zaidi na hata kuwazuia watu kufanya ibada ya misa katika dayosisi mbalimbali nchini humo.

Msemaji wa serikali ambae pia ni Waziri wa Habari, Lambert Mende, hakukawia kujibu matamshi ya Kadinali Mosengwo na kumtaka akumbuke kwamba mzozo uliopo haukuja kwa ajili ya kushindwa kutekelezwa kwa makubaliano ya Desemba 31 mwaka 2016.