GABON-SIASA

Bunge laondoa ukomo wa mihula kwa rais nchini Gabon

Wabunge nchini Gabon wamebadilisha Katiba ya nchi hiyo, na kuondoa ukomo wa mihula kwa rais, kinyume na ilivyokuwa awali ambapo alihudumu kwa mihula miwili, kila muhula miaka saba.

Ali Bongo Ondimba wakati wa mahojiano Libreville Gabon, Septemba 24, 2016.
Ali Bongo Ondimba wakati wa mahojiano Libreville Gabon, Septemba 24, 2016. REUTERS/Reuters TV
Matangazo ya kibiashara

Hii inamaanisha kuwa rais wa sasa Ali Bongo anaweza kusalia madarakani kwa muda mrefu iwapo atachaguliwa na raia wa nchi hiyo.

Rais ataendelea kuhudumu kwa muda wa miaka saba, lakini pia hawezi kufunguliwa mashtaka hata baada ya kuondoka madarakani.

Upinzani umepinga mabadiliko hayo, ambayo wamesema yanalenga kumsaidia rais Bongo kuendelea kuwa madarakani.

Tabia hii ya kubadili katiba imekua ni kawaida kwa viongozi wa Kiafrika wenye uchu wa madaraka.

Hali hii inashuhudiwa nchini Uganda, Burundi na nchi nyingine barani Afrika.

Wadadisi wanasema viongozi makatili ndio wanaonekana kufanya hivyo ili kuendelea kusalia madarakani hadi kufa kwao au wanapopinduliwa kama ilivyokua kwa alie kuwa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, rais wa Tunisia Zine el Abadine Ben Ali, Mobutu Sese Seko na wengineo.