UHISPANIA-CARLES-SIASA

Zoezi la kuapisha rais mpya wa Catalonia laahirishwa

Kaimu Spika wa Bunge la Cataloni Roger Torrent, tarehe 30 Januari 2018, Barcelona.
Kaimu Spika wa Bunge la Cataloni Roger Torrent, tarehe 30 Januari 2018, Barcelona. REUTERS/Rafael Marchante

Spika wa bunge la Catalonia ameamua leo Jumanne kuahirisha uzinduzi wa kikao cha kumuapisha Carles Puigdemont kama rais wa eneo hilo lakini alimtetea, akidai kwamba ana haki ya kutawazwa kama rais.

Matangazo ya kibiashara

"Kikao cha leo [...] kinaahirishwa" bila kutaja tarehe nyingine, alisema Roger Torrent baada kushtumu Mahakama ya Katiba, ambayo ilipiga marufu kuapishwa kwa Carles Puigdemont bila idhini ya mahakama, ni "kukiuka haki za mamilioni ya wananchi wa Catalonia ".

Kuwania nafasi hii kwa Carles Puigdemont ni matokeo ya "nia ya wengi katika bunge. Na wakati ambapo wingi huu umeendelea kuwa jinsi ulivyo, sintopendekeza mgombea mwingine yeyote, "aliongeza.

Bw Torrent alieleza kwamba lengo la kuahirishwa kwa zoezi hilo ni kutetea kuepo na mjadala kuhusu kuapishwa kwa Carles Puigdemont, bila kuepo na hatari ya kukamatwa.

Bw Puigdemont alikua uhamishoni kwa miezi mitatu mjini Brussels, ambapo alikimbia kukamatwa na serikali kuu ya Uhispania.