DRC-UCHAGUZI-SIASA

Corneille Nangaa: Zoezi la kuandika wapiga kura limemalizika vizuri

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi DRC, Corneille Nangaa Yobeluo (kushoto.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi DRC, Corneille Nangaa Yobeluo (kushoto. MONUSCO/Alain Wandimoyi

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Ucahguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (CENI), Corneille Nangaa, amesema zoezi la kuwaandika wapigakura katika nchi hiyo limetamatika vizuri mwishoni mwa mwezi wa Januari mwaka.

Matangazo ya kibiashara

Bw Nagaa ameelezea furaha yake kuona zoezi hilo lilimalizika kwa muda uliokuwa umepangwa.

Cornelle Nangaa ameikaribisha hatua hiyo ambayo amesema ni ya mwisho kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Desemba 23, 2018.

Hata hivyo amesema tatizo kubwa lililopo ni kuongezewa kwa wataalamu wa kimataifa ambao wameonyesha kutokuwa na imani na CENI.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya uchaguzi nchini DRC amesema tume yake iko huru na imekuwa ikiendelea kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kulingana na kalenda iliyotangazwa,