GUINEA-UCHAGUZI-SIASA

Matokeo ya uchaguzi kutangazwa Ijumaa hii Guinea Conakry

Rais wa Guinea Alpha Condé akipiga kura katika mji wa Conakry Jumapili (Februari 4) kwa uchaguzi wa serikali za mitaa.
Rais wa Guinea Alpha Condé akipiga kura katika mji wa Conakry Jumapili (Februari 4) kwa uchaguzi wa serikali za mitaa. CELLOU BINANI / AFP

Tume ya uchaguzi nchini Guinea Conakry imesema itatangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa serikali za mitaa hii leo ulioofanyika mwishoni mwa juma lililopita na kufuatiwa na vurugu ambapo watu zaidi ya 8 walipoteza maisha.

Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya hamsini wamekamatwa kuhusika ma matukio mbalimbali ya uhalifu wa baada ya uchaguzi huo ambao tume ya uchaguzi inalaumiwa kuchangia pakubwa.

Mkuu wa tume ya uchaguzi Salif Kebe amesema wako tayari kutangaza sehemu ya matokeo ya uchaguzi huo hii leo.

Hali ya utulivu imeendelea kushuhudiwa kwenye maeneo yaliyoshuhudia mapigano mwishoni mwa juma lililopita.

Waandamanaji wakiweka vizuizi kwenye barabara wakati wa makabiliano na polisi wa Guinea, Conakry tarehe 21 Novemba.
Waandamanaji wakiweka vizuizi kwenye barabara wakati wa makabiliano na polisi wa Guinea, Conakry tarehe 21 Novemba. CELLOU BINANI / AFP