AFRIKA KUSINI-SIASA-UCHUMI

Chama cha ANC kukutana kwa dharura

Cyril Ramaphosa (kulia), ambaye atamrithi Jacob Zuma (kulia) ikiwa atajiuzulu kwenye wadhifa wa rais, hata hivyo anakabiliwa na vikwazo viwili vikubwa ili kumaliza kabisa mgogoro huu
Cyril Ramaphosa (kulia), ambaye atamrithi Jacob Zuma (kulia) ikiwa atajiuzulu kwenye wadhifa wa rais, hata hivyo anakabiliwa na vikwazo viwili vikubwa ili kumaliza kabisa mgogoro huu REUTERS/Siphiwe Sibeko/File Photo

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congres (ANC) kinatarajia kukutana kwa dharura hivi leo Jumatatu ili kumalizia suala muhimu la kuondoka madarakani kwa Rais Jacob Zuma, kwa mujibu wa kiongozi wa chama hicho Cyril Ramaphosa.

Matangazo ya kibiashara

Rais Zuma na Bw Ramaphosa walikutana kwa mazungumzo Februari 6 ili kutatua tatizo hili la tete, lakini mazungumzo bado yanaendelea.

Leo Jumatatu, taaisisi kuu yenye maamuzi ya ANC, Kamati kuu ya chama katika ngazi ya kitaifa (NEC), ambayo iliamuru Cyril Ramaphosa kujadiliana na Rais Zuma, inatarajia kukutana kwa faragha hii leo Jumatatu.

"Raia wetu wanataka suala hili limalizike, hatua hii ndio inatazamiwa kutekelezwa na kamati kuu ya chama katika ngazi ya kitaifa (NEC) leo Jumatatu mjini Pretoria", alisema siku ya Jumapili Cyril Ramaphosa, bila kutoa maelezo zaidi.

"Tunajua kwamba mnataka mabadiliko," alisema Makamu wa Rais siku ya Jumapili mbele ya maelfu ya wafuasi wa ANC waliokusanyika mjini Cape Town, kusini magharibi mwa nchi, wakati wa kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwa Nelson Mandela, baba wa taifa.

Cyril Ramaphosa, ambaye atamrithi Jacob Zuma ikiwa atajiuzulu kwenye wadhifa wa rais, hata hivyo anakabiliwa na vikwazo viwili vikubwa ili kumaliza kabisa mgogoro huu: kupinga kwa rais Zuma kung'atuka madarakani, na mgawanyiko katika chama cha ANC.

Mnamo Februari 4, Jacob Zuma alikataa kujiuzulu, licha ya shinikizo kutoa kwenye uongozi wake wa chama.

Katika mazungumzo yanayoendelea, Jacob Zum anataka apewe kinga ya kutofuatiliwa na vyombo vya sheria, wakati ambapo jina lake linarejea katika kesi nyingi za rushwa. Pia anatafuta kupata huduma ya gharama zake za kisheria, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo siku ya Jumapili, Cyril Ramaphosa, alisema wazi kwamba