AFRIKA KUSINI-SIASA-UCHUMI

ANC yampa Jacob Zuma saa 48 kuwa amejiuzulu

Wanachama wa ANC mbele ya makao makuu ya chama Johannesburg kutaka Rais Jacob Zuma ajiuzulu.
Wanachama wa ANC mbele ya makao makuu ya chama Johannesburg kutaka Rais Jacob Zuma ajiuzulu. MARCO LONGARI / AFP

Chama tawala nchini Afrika Kusini, African National Congress (ANC) kimeamua kumpa Rais Jacob Zuma saa 48 kuwa amejiuzulu kama rais wa Afrika Kusini, runinga ya SABC imeripoti ikinukuu vyanzo vingi siku ya Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka chama cha ANC, ANC ilifanya mazungumzo marefu baadaye kuwatuma watu wawili nyumbani kwa Rais Zuma jijini Pretoria kwenda kumfikishia ujumbe wa chama ana kwa ana ya kwamba Zuma ajiuzulu mwenyewe au chama kimng'oe madarakani.

Rais wa ANC Cyril Ramaphosa alitoka mkutanoni uliokua uliitishwa na Kamati Kuu ya chama (NEC) saa 22:30 (sawa na saa 20:30 saa za kimataifa) ili kumjulisha Jacob Zuma kuhusu uamuzi huo, SABC imeongeza.

Mkutano huo uliyofanyika katika hoteli ya mjini Pretoria ulidumu saa nane.

Msafara wa magari yaliyombeba Ramaphosa ulirudi saa moja baadaye.

Jacob Zuma, ambaye mwenye umri wa miaka 75, anakabiliwa na mfululizo wa kesi za rushwa tangu kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi mwaka 2009. Tayari amepoteza nafasi yake kama kiongozi wa ANC. Nafas yake ilichukuliwa mwezi Desemba na Makamu wake Cyril Ramaphosa.

Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa anaongoza shinikizo za kumuondoa Zuma katika nafasi yake hiyo ya Urais, na hatimaye kushika pia nafasi hiyo.

Ramaphosa ameahidi pia kupambana na rushwa iliyokithiri na kukijenga upya chama cha ANC, wakati nchi hiyo ikielekea katika uchaguzi mwakani.

Kamati Kuu ya cahama cha ANC ina uwezo wa kuomba kujiuzulu kwa Jacob Zuma.