ISRAEL-UCHUMI-UFISADI

Polisi ya Israel yaamuru Benjamin Netanyahu achunguzwe

Benjamin Netanyahu akitoa hotuba yake kwenye televisheni ya Israel tarehe 13 Februari 2018.
Benjamin Netanyahu akitoa hotuba yake kwenye televisheni ya Israel tarehe 13 Februari 2018. Israeli Pool/via REUTERS

Waziri Mkuu wa Israel anakabiliwa na makosa mawili ya rushwa na kuvunjwa uaminifu. Wachunguzi wanaamini kwamba wamepata ushahidi wa kutosha wa kumshtaki Waziri Mkuu Netanyahu katika kesi hizi mbili. Siku ya Jumanne Bw Netanyahu, kwa upande wake, alirudia tena kujitetea akisema hajavunja sheria yoyote.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni hali ngumu zaidi kwa Benjamin Netanyahu. Polisi wanaamini wamepata ushahidi wa kutosha ili kumfungulia mashtaka. Katika kesi zote mbili, polisi wanasisitiza makosa matatu: rushwa, udanganyifu na kuvunjwa uaminifu.

Katika kesi ya kwanza, wachunguzi wanabaini kwamba Benjamin Netanyahu alikubali zawadi yenye thamini isiyo halali kutoka kwa wafanyabiashara wawili matajiri. Ni kuhusu sigara na chupa za mvinyu kwa jumla ya kitita cha mamilioni ya euro.

Katika kesi ya pili, mbele ya polisi, Benjamin Netanyahu amejaribu kujadiliana na mmiliki wa gazeti kuu nchini Israel, Yediot Aharonot.

Waziri mkuu wa Israel anatuhumiwa kwa kutaka gazeti la nchi hiyo la Yediot Aharonot kuchapisha taarifa yake kwa upendeleo, ikiwa kama takrima kulisaidia kuweza kudhibiti magazeti yanayoshindana nayo.

Polisi wanasema mhariri wa gazeti hilo Arnon Mozes naye pia anapaswa kushtakiwa.

Tangu mwanzo wa uchunguzi huu, Benjamin Netanyahu amekua akisema mara kwa mara kwamba hakufanya chochote kibaya.

Akizungumza kupitia Televisheni ya Israel, Benjamin Netanyahu amesema madau hayo hayana msingi wowote na ataendelea kuwa Waziri mkuu wa nchi hiyo.