AFRIKA KUSINI-SIASA-UCHUMI

Raia wa Afrika Kusini wasubiri uamuzi wa Zuma juu ya kujiuzulu

RAis wa Afrika Kusini Jacob Zuma katika kikao cha Bunge, Cap, Novemba 2, 2017.
RAis wa Afrika Kusini Jacob Zuma katika kikao cha Bunge, Cap, Novemba 2, 2017. REUTERS/Sumaya Hisham

Wananchi wa Afrika Kusini wanasubiri kwa hamu na gamu jibu la rais wao Jacob Zuma kuhusu kujiuzulu kwake au la kwenye wadhifa wake, baada ya chama chake kumtaka aachie ngazi.

Matangazo ya kibiashara

ana Jumanne chama tawala nchini Afrika Kusini ANC, kilimpa rasmi barua rais Jacob Zuma kikimtaka kujiuzulu nafasi yake.

Katibu Mkuu wa chama hicho Ace Magashule amesema baada ya majadiliano yaliyoenda mpaka usiku wa kuamkia jana Jumanne, kamati kuu iliamua kumuandikia barua rais Zuma kumtaka ajiuzulu nafasi yake lakini bila kumpa muda maalumu.

Tangu kuchukua hatamu ya uongozi wa chama mwezi Desemba, Makamu wa rais, Cyril Ramaphosa, amekua akishinikiza Rais Zuma aachie ngazi, baada ya kukabiliwa na kesi za rushwa, ili kuepuka chama cha ANC kisije kupoteza katika uchaguzi mkuu wa 2019 .

Baada ya wiki kadhaa za mazungumzo na majadiliano, uongozi wa ANC hatimaye uliamua siku ya Jumanne kuomba Rais Zuma ajiuzulu.

Katibu mkuu wa chama, Ace Magashule, amethibitisha kwamba rais "amekubali kanuni ya kuachia madaraka" lakini kwa masharti yake, kwa muda wa miezi mitatu hadi sita, masharti ambayo hayakubaliki na ANC.