AFRIKA KUSINI-SIASA-UCHUMI

Ramaphosa kumrithi mtangulizi wake Afrika Kusini

Jacob Zuma (kushoto) na Cyril Ramaphosa,Desmba 16, 2017,  Johannesburg Afrika Kusini.
Jacob Zuma (kushoto) na Cyril Ramaphosa,Desmba 16, 2017, Johannesburg Afrika Kusini. REUTERS/Siphiwe Sibeko/File Photo

Nchi ya Afrika Kusini inatarajia kumpata rais wake mpya ambaye ni Makamu wa rais, Cyril Ramaphosa, mwenye umri wa miaka 65, siku moja tu baada ya kujiuzulu kwa mtangulizi wake Jacob Zuma baada ya chma chake cha ANC kumtaka ajiuzulu.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa Zuma kujiuluzu ulikuja baada ya wiki kadhaa majadiliano makali na chama chake, African National Congress (ANC).

Bw Zum aambaye anaendelea kukabiliwa na kashfa ya rushwa, alitangaza kujiuzulu jana Jumatano usiku, baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka tisa.

Mapema jana Jumatao Jacob Zuma alikataa kutii amri ya chama chake kikimtaka ajiuzulu, kabla ya chama hicho kutishia kuwasilisa bungeni hivi leo muswada wa kutokua na imani dhidi yake.

"Nimeamua kujiuzulu kwenye nafasi ya rais wa Jamhuri kwa haraka, hata kama sikubaliani na uamuzi wa uongozi wa chama changu," alisema Zuma katika hotuba iliyodumu saa moja na nusu, hotuba iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni nchini Afrika Kusini.

Cyril Ramaphosa, mfanyabiasaha wa zamani, aliyechaguliwa kama kiongozi wa chama cha ANC tangu mwezi Desemba mwaka jana, anatazamiwa kupigiwa kura na bunge ili kumrithi mtangulizi wake leo Alhamisi au kesho Ijumaa.

Kwa wiki kadhaa, Cyril RAmaphosa alikuwa akijaribu kumsihi mtangulizi wake kuondoka madarakani kwa upole, kufuatia kashfa za rushwa zinazomkabili, ili kuepuka kushindwa kwa chama cha ANC katika uchaguzi wa mwaka 2019.

Muhula wa Jacob Zuma ungelimalizika mwaka kesho.

Zuma aliyezaliwa katika familia masikini na baadae kuishi uhamishoni sababu ya kupinga ubaguzi wa rangi kabla ya kupanda ngazi na kushika hatamu kama rais wa watu, anaendelea kukabiliwa na kashfa mbalimbali.

Zuma alituhumiwa kumbaka rafiki wa familia yake ambaye anaishi na virusi vya ukimwi mwaka 2006, lakini licha ushaidi Zuma aliambia mahakama kuwa alioga ili kujikinga na kupata virusi vya ukimwi ambavyo vinge muandama muda wote wa uraisi wake.

Mara zote Zuma amekanusha tuhuma hizo na kuapa kuachia ngazi ikithibitika kama ni kweli amehusika.