VENEZUELA-SIASA

Upinzani kutoshiriki uchaguzi wa urais nchini Venezuela

Nicolas Maduro atapambana katika uchaguzi huo na Mchungaji javier Bertucci (kwenye picha), ambaye hana umaarufu wowote nchini Venezuela.
Nicolas Maduro atapambana katika uchaguzi huo na Mchungaji javier Bertucci (kwenye picha), ambaye hana umaarufu wowote nchini Venezuela. REUTERS/Marco Bello

Muungano wa upinzani nchini Venezuela umetangaza kwamba hautoshiriki uchaguzi wa rais ambao umepangwa kufanyika Aprili 22, uchaguzi ambao upinzani unasema "ni kinyume cha sheria" na utagubikwa na "udanganyifu".

Matangazo ya kibiashara

Muungano huo wa upinzani unasema unasikitishwa hasa na mazingira ya maandalizi ya uchaguzi huo.

Hatua hii ya upinzani kujitoa katika kinyang'anyiro hiki cha urais, inampa na fasi kubwa rais anayemaliza muda wake, Nicolas Maduro, kushinda uchaguzi huo.

Wapinzani wake wawili, Leopoldo Lopez na Henrique Capriles, hawataweza kukuwania katika uchaguzi huo. Bw Lopez anakabiliwa na kifungo cha nyumbani. Naye Bw Capriles hana haki ya kuwania kutokana na tuhuma za ubadhirifu anazohtumiwakwa alipokua Mkuu wa mkoa.

Muungano mkuu wa upinzani, MUD, hauna haki yoyote ya kuteua mgombea mmoja, Mahakama Kuu ilitangaza hivi karibuni.

Kwa sasa, Nicolas Maduro hana mpinzani yoyote anayemtisha katika uchaguzi huo. Nicolas Maduro anapambana katika uchaguzi huo na Mchungaji javier Bertucci, ambaye hana umaarufu wowote nchini Venezuela.