MAREKANI-EU-KODI-UCHUMI

Ushuru wa Marekani: Umoja wa Ulaya yaahadi kujibu

Umoja wa Ulaya hauwezi kubaki hivyo bila kujibu, ameonya Jean-Claude Juncker baada ya kupata uthibitisho kuhusu kodi za Marekani.
Umoja wa Ulaya hauwezi kubaki hivyo bila kujibu, ameonya Jean-Claude Juncker baada ya kupata uthibitisho kuhusu kodi za Marekani. REUTERS/Dado Ruvic

Kiwango cha utozaji ushuru mkubwa wa Marekani unaanza kutekelezwa leo wakati huu mataifa mbalimbali duniani yakiendelea kulaani utawala wa rais Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi kutoka mataifa yaliyoathiriwa na hatua hiyo ya Rais Donald Trump wameipokea kwa ukali, huku na wao wakiweka ushuru mkubwa hususan kwa vito vinavyotoka Marekani, wakianzia chuma kwenda kwenye mifuko ya kulalia na kalamu.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemuambia rais Trump kwa njia ya simu kwamba uamuzi huo upo kinyume cha sheria kabla ya kuongeza kuwa Umoja wa Ulaya (EU) ungeweza kujibu kwa "njia imara na ya uwiano"

Rais Macron amekuwa na uhusiano mzuri na kiongozi huyo wa Marekani.

Rais Trump ametetea uamuzi wake huo akisema haki za ushuru kwa wazalishaji wa chuma na wa aluminium wa Marekani ni muhimu kwa usalama wa taifa wanaotishiwa na masoko ya kimataifa.

Mtazamo huo wa Rais Trump umetupiliwa mbali na washirika wake. Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau ameelezea madai hayo kama chuki binafasi na kwamba Canada haiwezi kuonekana kuwa tishio kwa usalama wa Marekani.