MOROCCO-UCHUMI-SIASA

Waziri ajiuzulu kufuatia hali mbaya ya kiuchumi Morocco

Danone, mojawapo ya bidhaa za kampuni zilizolengwa na wito wa kususiwa Morocco.
Danone, mojawapo ya bidhaa za kampuni zilizolengwa na wito wa kususiwa Morocco. Yuri KADOBNOV/AFP

Waziri wa Utawala Bora wa Morocco Lahcen Daoudi amewasilisha barua yake ya kujiuzulu, baada ya kukosolewa kufuatia kushiriki kwake katika maandamano dhidi ya mfumko wa bei, hasa kwa bidhaa za kampuni ya Danone nchini Morocco.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha kiislamu cha PJD, kinachoongoza serikali ya muungano, kimetangaza kuwa Bw Daoudi, moja wa vigogo wa muungano huo, amewasilisha barua yake ya kujiuzulu wakati wa mkutano wa dharura wa chama cha PJD uliofanyika Jumatano jioni wiki hii.

Katika taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo, uliyoongozwa na Waziri Mkuu na kiongozi wa chama cha PJD Saadeddine Othmani, chama cha PJD kimepokea "ombi" la Daoudi kujiuzulu na nafasi yake kuchukuliwa na mtu mwengine baada ya kushiriki mgomo Jumatano jioni mbele ya jengo la Bunge".

Bw Daoudi, mwenye umri wa miaka 71, alishiriki kwenye mstari wa mbele wakati wa mgomo wa wafanyakazi wa kampuni tanzu ya Morocco mjini Danone, ambao waliandamana siku ya Jumanne jioni wiki hii wakielezea hofu yao ya kupoteza ajira, wakati ambapo kampuni hii inakabiliwa na mgomo wa kipekee.

Kushiriki mgomo huo kwa Bw Daoudi kulizua mjadala kwa siku ya Jumatano katika vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii nchini Morocco. Waziri Mkuu anatarajia kuwasilisha ombi la kujiuzulu la Bw Daoudi kwa mfalme ili kusahihishwa.