CANADA-G7-BIASHARA-UCHUMI

Mkutano wa mataifa tajiri duniani G7 kuanza Canada

Vizuizi vya usalama vilivyowekwa karibu na jengo ambako la Richelieu, ambako kunatarajiwa kufanyika mkutano wa mataifa tajiri duniani G7, Canada.
Vizuizi vya usalama vilivyowekwa karibu na jengo ambako la Richelieu, ambako kunatarajiwa kufanyika mkutano wa mataifa tajiri duniani G7, Canada. REUTERS/Yves Herman

Viongozi kutoka mataifa ya G 7 yenye uchumi mkubwa duniani, wanakutana mjini Quebec nchini Canada. Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea mkutano huo.

Matangazo ya kibiashara

Ni mkutano unaofanyika Ijumaa na Jumamosi wiki hii huku Marekani ikionekana kutengwa kutokana na sera yake ya kibiashara dhidi ya Mataifa ya Magharibi.

Kitendo cha Trump kuongeza ushuru katika bidhaa za chuma kumemuweka katika mazingira ya kutofautiana na mataifa wanachama wa G7.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema, mataifa sita hayataona aya ya kutia saini mkataba wowote bila ya Marekani.

Hata hivyo Rais Macron aliwaambia waandishi wa habari kwamba watatumia mkutano ujao wa G7 kumshawishi rais Trump dhidi ya msimamo wake kibiashara.

Rais wa Marekani Donald Trump anakwenda katika mkutano huu na sera ya Marekani kwanza, baada ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za vyuma na Alluminium vinavyoingizwa nchini humo kutoka mataifa ya Ulaya.

G7 inaundwa na Marekan, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Uingereza.