CHINA-MAREKANI-BIASHARA

Vita vya kibiashara kati ya China na Marekani vyaanza

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imetangaza siku ya Ijumaa bila maelezo zaidi kwamba ushuru umeanza kutumika dhidi ya bidhaa za Marekani.
Wizara ya Mambo ya Nje ya China imetangaza siku ya Ijumaa bila maelezo zaidi kwamba ushuru umeanza kutumika dhidi ya bidhaa za Marekani. REUTERS/Jason Lee

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imetangaza Ijumaa wiki hii bila maelezo zaidi kwamba ushuru umeanza kutumika dhidi ya bidhaa za Marekani

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Wizara hiyo, Lu Kang, amesema maafisa wa forodha wameanza kutekeleza hatua hiyo kutoza ushuru bidhaa hizo, kukabiliana na kuanza kutumika nchini Marekani kwa ushuru kuhusu bidhaa zinazotoka China.

Ameongeza, katika wa mkutano na waandishi wa habari, kwamba shinikizo kutoka upande mmoja utaonekana halina maana na China bado inapinga msuala linalochukuliwa na upande mmoja na suala la kulinda biashara.

Ushuru wa Marekani kwa bidhaa kutoka China zenye thamani ya dola bilioni 34 umeanza kutumika Ijumaa hii alfajiri (saa 04:01).

Vita vya kibiashara yvilivyoanzishwa na utawala wa Donald trump vinaweza kuongezeka, kwa kuwa Donald Trump amesikika akisema kuwa Washington inatarajia kutoza bidhaa kutoka China hadi dola bilioni 500, sawa na bidhaa zote zinazotengenezwa China nchini Marekani (dola bilioni 505 mwaka 2017).