EU-MAREKANI-CHINA-BIASHARA-UCHUMI

Biashara: EU yaomba China, Urusi na Marekani "kuepukana na uhasama"

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk.
Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk. REUTERS/Eric Vidal

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk ametolea mwito China "kuepukana na uhasama" wa vita vya biashara, kama alivyomjibu Donald Trump ambaye aliutaja Umoja wa Ulaya (EU), China na Urusi kwamba ni maadui.

Matangazo ya kibiashara

"Bado wakati upo wa kuepukana na uhasama na machafuko," Tusk amesema katika mkutano na Waziri Mkuu wa China Li Keqiang, akitaka kuanza marekebisho kwenye Shirika la Biashara Duniani (WTO) .

"Sisi sote tunafahamu kwamba picha ya ulimwengu imeanza kubadilika tukishuhudia," amesema Tusk, akikumbusha kuwa "dunia ambayo imejengwa kwa miaka mingi (...) imepelekea Ulaya kuwa na amani, maendeleo ya China na mwisho wa vita baridi ".

"Ni wajibu wa kila mmoja, Ulaya na China, lakini pia Marekani na Urusi, kutoharibu dunia hii bali badala yake inatakiwa kuboreshwa, na kuepuka vita vya biashara ambavyo vimeibuka kufuatia migogoro ya mara kwa mara katika historia yetu, "almesema Tusk, saa machache kabla ya mkutano wa kwanza kati ya Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin huko Helsinki.

Wito wa maelewano unaofanana na taarifa za karibuni za Donald Trump. Katika mahojiano siku ya Jumapili, rais wa Marekani alisema kuwa Urusi, Umoja wa Ulaya na China, kwa sababu mbalimbali.