UGIRIKI-UCHUMI

Ugiriki yaachana na mpango wa kukopeshwa fedha kuhusu uchumi wake

Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras akikutana na wajumbe wa baraza lake la mawazir Athens Aprili 3, 2018.
Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras akikutana na wajumbe wa baraza lake la mawazir Athens Aprili 3, 2018. REUTERS/Costas Baltas

Ugiriki imefanikiwa kujiondoa kwenye mpango wa Umoja wa Ulaya wa kukopeshwa fedha ili kuimarisha uchumi wake. Ugiriki imejiondoa katika hali hiyo baada ya miaka mitatu ya mahangaiko ya kiuchumi.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mara ya kwanza, ndani ya miaka minane, Ugiriki sasa inakuwa huru kukopa kupitia masoko yake ya kifedha.

Umoja wa Ulaya, ulikuwa umeipa Ugiriki mkopo wa Dola Bilioni 70 kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ili kuisaidia katika uchumi wake uliokuwa umeyumba, hatua ambayo iliisababisha nchi hiyo kutangaza ubanaji wa matumizi ya fedha, ambao haukuwafurahisha wananchi.

Katika kipindi hicho, uchumi wa Ugiriki umekuwa ukikua taratibu na kwa hatua hii, inaaminiwa kuwa hali itaimarika huku mpango wa kubana matumizi ya fedha ukiondolewa.