AFRIKA-CHINA-UCHUMI-MAENDELEO

China yaahidi kutoa dola Bilioni 60 kwa maendeleo ya Afrika

Rais wa China Xi Jinping katika sherehe ya ufunguzi wa kongamano la kiuchumi  kati ya China na Afrika katika Kituo cha Makumbusho cha Beijing, Septemba 3, 2018.
Rais wa China Xi Jinping katika sherehe ya ufunguzi wa kongamano la kiuchumi kati ya China na Afrika katika Kituo cha Makumbusho cha Beijing, Septemba 3, 2018. © AFP

China itatoa zaidi ya dola bilioni 60 kwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi za Afrika, Rais wa nchi hiyo, Xi Jinping, ameahidi Jumatatu wiki hii wakati wa ufunguzi wa kongamano la kiuchimi kati ya China na Afrika huko Beijing.

Matangazo ya kibiashara

Msaada huyo kutoka China kwa Afrika utajumuisha dola bilioni 15 za "misaada ya bure na mikopo isiyo na riba," Xi amesema, wakati Beijing inashtumiwa kutoa madeni kwa washirika wake kwa njia ya mikopo ya gharama kubwa.

Xi Jinping amesema, lakini bila kufafanua ratiba au orodha ya nchi husika, kwamba China inatarajia "kufuta" sehemu ya madeni kwa nchi zenye maendeleo ya chini barani Afrika.

Xi Jinping amebaini kwamba makampuni ya China yatatakiwa kuwekeza "angalau dola bilioni 10" barani Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Katika mkutano wa awali kati ya China na Afrika huko Johannesburg, nchini Afrika Kusini, mwaka wa 2015, Xi Jinping alitangaza kwamba nchi yake itatoa msaada wa dola Bilioni 60 na mikopo kwa nchi za Afrika.