Tume Huru ya Uchaguzi DRC, CENI yatangaza majina ya wagombea Urais

Sauti 10:04
Mwenyekiti wa  Céni, DRC, Corneille Nangaa
Mwenyekiti wa Céni, DRC, Corneille Nangaa © JOHN WESSELS / AFP

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi CENI nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC, Corneille Nangaa ametangaza majina ya wagombea urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Disemba 23 mwaka huu huku wanasiasa wa upinzani Jean Pierre Bemba na mwenzake Moise Katumbi wakikosa nafasi ya kugombea kutokana na sababu mbalimbali. Je unataka kujua nguvu ya upinzani inasimama katika nafasi gani? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala haya ya Wimbi la Siasa.