MAREKANI-CANADA-BIASHARA-UCHUMI

Marekani na Canada wafikia mkataba mpya wa kibiashara

Rais wa Marekani Donald Trump (kulia) na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau Washington, DC, Oktoba 11, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump (kulia) na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau Washington, DC, Oktoba 11, 2017. REUTERS/Jonathan Ernst

Baada ya zaidi ya mwaka wa mazungumzo, hatimaye Canada na Marekani wameafikiana kutia saini kwenye mkataba mpya wa biashara, AEUMC, ambao pia unaihusisha Mexico.

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo yalifanyika hadi muda wa mwisho uliyowekwa na Rais Donald Trump kwa kufuta makubaliano hayo. Muda huo ulikuwa uliwekwa hadi Jumapili usiku wa manane, saa za Marekani.

Canada itanufaika kwenye mkataba huo. Karibu theluthi tatu ya bidhaa zinazotengenezwa nchini Canada zitaingizwa nchini Marekani. Jambo muhimu kwa Canada ilikuwa kuweka mfumo wa utatuzi wa migogoro.

Mfumo huu unaruhusu mmoja wa washirika kupinga kodi itakayowekwa bila mwafaka na nchi nyingine.

Rais Trump alikuwa anataka kufuta hatua hii, ambayo iliruhusu Canada kunufaika zaidi kupitia Marekani.

Kwa upande mwingine, ushuru mkubwa uliowekwa kwenye bidhaa za chuma na bati kutoka Canada miongoni mwa mengine na Rais Donald Trump kwa lengo la kulinda sekta ya chuma ya Marekani utabaki, licha ya Canada kulalama.