AFRIKA KUSINI-UCHUMI-SIASA

Chama cha EFF chafutilia mbali shutma dhidi yake kuhusu kashfa ya benki Afrika Kusini

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF), Julius Malema,katika mkutano na waandishi wa habari Johannesburg, Oktoba 16, 2018.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF), Julius Malema,katika mkutano na waandishi wa habari Johannesburg, Oktoba 16, 2018. GIANLUIGI GUERCIA / AFP

Chama cha upinzani chenye msimamo mkali nchini Afrika Kusini cha EFF kimekanusha madai ya kuhusika kwake katika kashfa ya ubadhirifu katika benki moja nchini humo, na kushtumu hoja zakisiasa zisizoeleweka miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu.

Matangazo ya kibiashara

"Chama cha EFF hakihusiki na makosa yoyote ya ubadhirifu," amesema Julius Malema kiongozi wa chama hicho.

"Baadhi wanataka kuchafulia jina chama cha EFF ili kiweze kupoteza sehemu ya wafuasi wake katika uchaguzi wa mwaka 2019," Malema mesema katika mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama chake huko Johannesburg.

Wiki iliyopita, ripoti iliyoombwa na Benki Kuu ya taifa nchini humo ilibainisha kuwa akaunti za VBS Mutual, maarufu kwa kutoa mkopo kwa Rais wa zamani Jacob Zuma, zilichukuliwa fedha kwa udanganyifu zinazo kadiriwa sawa na euro milioni 110.

Naibu kiongozi wa chama cha EFF, Floyd Shivambu, anashtumiwa, pamoja na nduguye, kuwa mmojawapo wa watu "waliopitisha mlango wa nyuma fedha hizo".

"Hatujapata pesa kutoka kwa akaunti za VBS na wale wanaofikiria kuwa hali hiyo ilitokea ni wendawazimu," Shivambu amesema Jumanne wiki hii.

Wajumbe kadhaa wa chama tawala cha African National Congress (ANC) pia wamehusishwa katika kesi hiyo.