BENKI UA DUNI-UCHUMI

Rais wa Benki ya Dunia ajiuzulu

Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim, hapa ilikuwa Novemba 6, 2018 Beijing.
Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim, hapa ilikuwa Novemba 6, 2018 Beijing. REUTERS/Thomas Peter

Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim ametangaza kuwa, atajizulu wadhifa huo mwezi ujao, miaka mitatu kabla ya muda wake kumalizika.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inatarajiwa kumpa Rais wa Marekani Donald Trump, fursa ya kushawishi kiongozi mpya wa Benki inayolenga kumaliza umasikini duniani.

Chini ya uongozi wake, Kim alikuwa amejiwekea malengo ya Benki hiyo kumaliza umasikini kufikia mwaka 2030.

Katika taarifa yake, Jim Yong Kim, ambaye amekuwa akiongoza Benki ya Dunia kwa miaka sita, amesema tu kwamba atajiunga na "kampuni ya uwekezaji" na kuzingatia "uwekezaji wa miundombinu katika nchi zinazoendelea."