MAREKANI-TRUMP-DAVOS-UCHUMI

Trump afuta ziara ya ujumbe wa nchi yake Davos

Rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump. REUTERS/Jim Young

Rais wa Marekani Donald Trump, amefuta ziara ya ujumbe wa Marekani katika mkutano wa dunia wa kiuchumi mjini Davos, lakini pia amemzuia Spika wa bunge Nancy Pelosi kuzuru nchi za Ubelgiji na Misri ikiwa ni pamoja na kwenda nchini Afganistan.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imechukuliwa na rais Trump kufuatia kukwama kwa shuguli za serikali, baada ya bunge kukataa kupitisha bajeti na kusababisha zaidi ya wafanyakazi Laki nane, kutopata mishahara yao.

Msemaji wa Ikulu ya White house Sarah Sanders amesema, ujumbe huo hauwezi kwenda kuhudhuria mkutano huo unaoanza wiki ijayo hadi pale mwafaka utakapopatikana.

Rais Trump mwenyewe alitarajiwa kuhudhuria mkutano huo lakini mvutano huu umesababisha asalie nyumbani.

Mbalia na Afgnistan, Pelosi alitarajiwa kuzuru Brussels Ubelgiji, na Cairo Misri katika ziara ya kikazi, ziara ambayo Trump sasa anasema itafanyika tu hadi pale wabunge wa Democratic watakaporuhusu kupitishwa kwa bajeti ambayo itamwezesha rais Trump kuanza kujenga ukuta kati ya nchi hiyo na Mexico, suala ambalo wabunge wa Democratic ambao ni wengi bungeni wanasisitiza hawatakubali.