MSUMBIJI-RUSHWA-UCHUMI

Msumbiji: Mtoto wa rais wa zamani akamatwa kwa kosa la rushwa

Mji mkuu wa Msumbiji, Maputo, Juni 24 2015, katika mkesha wa maadhimisho ya miaka 40 ya uhuru wa nchi hiyo kutoka mikononi mwa Wareno (picha ya kumbukumbu).
Mji mkuu wa Msumbiji, Maputo, Juni 24 2015, katika mkesha wa maadhimisho ya miaka 40 ya uhuru wa nchi hiyo kutoka mikononi mwa Wareno (picha ya kumbukumbu). ADRIEN BARBIER / AFP

Ndambi Guebuza, mtoto wa kwanza kati ya watoto wanne wa rais wa zamani wa Msumbiji Armando Guebuza anazuiliwa tangu mwishoni mwa wiki hii iliyopita nchini Msumbiji.

Matangazo ya kibiashara

Ndambi Guebuza alikamatwa akiwa nyumbani kwake katika uchunguzi kuhusu mtandao wa rushwa aliotumia kwa kuchukuwa "deni lililofichwa" la taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusu deni hilo "lililofichwa".

Kashfa hiyo ya rushwa ilianza miaka kumi iliyopita. Serikali ya Maputo imekuwa ikichukuwa mikopo kupitia makampuni ya umma kwa zaidi ya dola Bilioni mbili. Kiwango hiki ni kikubwa ukitalinganisha na pato la Taifa la Msumbiji. Pato hilo kwa sasa linakaribia dola Bilioni 16. Mikopo hutolewa na Bunge pamoja na wakopaji wa kimataifa.

Fedha hizi zinawezesha kununua meli, vyombo mbalimbali vya kusafiria, lakini pia meli za kijeshi, vifaa ambavyo kwa sehemu mmoja vimetengenezwa nchini Ufaransa.

Lakini siri hiyo haijafichwa kwa muda mrefu. Mnamo mwaka 2016, "deni hilo lililofichwa" lilidhihirika siku moja na wakati huo uchumi wa Msumbiji ulijikuta pabaya. Nchi hiyo inakabiliwa na mdororo wa kifedha tangu ilipopata uhuru wake. Wengi wa wafadhili wamesitisha misaada yao na serikali ya Maputo italazimika kusitisha zoezi la kulipa madeni yake. Kwa leo sasa, serikali inajaribu kuomba tena mazungumzo na wafadhili wake.

Mashirika yasiyo ya kiserikali yanakataa serikali kulipa "madeni yaliyofichwa" kutokana na kuwa bado kuna mashaka makubwa kuhusu matumizi ya fedha hizo.