Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-UCHUMI-MAANDAMANO

Sudan: Fedha nyingi zakamatwa katika nyumba ya al-Bashir

Kiongozi wa Baraza la kijeshi, Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, alithibitishia maafisa wa polisi, jeshi kwamba kuligunduliwa euro milioni saba, Dola laki 3 na 50,000 na pesa bilioni tano za Sudan. Kwa ujumla, ni zaidi ya euro milioni 100.
Kiongozi wa Baraza la kijeshi, Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, alithibitishia maafisa wa polisi, jeshi kwamba kuligunduliwa euro milioni saba, Dola laki 3 na 50,000 na pesa bilioni tano za Sudan. Kwa ujumla, ni zaidi ya euro milioni 100. ASHRAF SHAZLY / AFP

Wakati waandamanaji wakiendelea kupiga kambi mbele ya makao makuu ya jeshi jijini Khartoum tangu Aprili 6, kiongozi wa Baraza la mpito la kijeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, amefanya mahojiano yake ya kwanza ya televisheni.

Matangazo ya kibiashara

Ameelezea nia ya baraza lake la kukabidhi madaraka kwa raia na kuahidi kwamba jeshi bila shaka, litajibu madai ya waandamanaji wiki.

Wakati huo huo Bw Burhan pia ametangaza kwamba wamekamata fedha nyingi katika nyumba ya Omar El Bashir aliyetimuliwa madarakani tarehe 11 Aprili mwaka huu.

Tangu Jumamosi, video imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ikionesha mirundo ya manoti ya fedha katika moja ya makaazi ya Omar Hassan al-Bashir.

Siku ya Jumapili, kiongozi wa Baraza la kijeshi, Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, alithibitishia maafisa wa polisi, jeshi kwamba kuligunduliwa euro milioni saba, Dola laki 3 na 50,000 na pesa bilioni tano za Sudan ... Kwa ujumla, ni zaidi ya euro milioni 100.

Wakati huo huo waangalizi wamebaini kwamba Mwendesha mashtaka anachunguza madai ya Utakasishaji wa Fedha Haramu dhidi ya Omar al-Bashir.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.