CHINA-MAREKANI-IMF-BIASHARA-UCHUMI

Biashara: Mkurugenzi wa IMF aonya China na Marekani

Wawakilishi wa China na Marekani wanatarajia kukutana mwishoni mwa wiki hii jijini Washington, nchini Marekani, kwa mkutano mkubwa kuhusu mvutano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Mkurugenzi Mkuu wa IMF Christine Lagarde katika mkutano na waandishi wa habari kando na Mkutano wa Paris kuhusu madeni na maendeleo, Mei 7, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa IMF Christine Lagarde katika mkutano na waandishi wa habari kando na Mkutano wa Paris kuhusu madeni na maendeleo, Mei 7, 2019. REUTERS/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Hali si shwari baada ya rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuongeza kodi ya dola bilioni 200 kwa bidhaa kutoka China.

Mkurugenzi Mkuu wa IMF Christine Lagarde amesema mvutano wa kibiashara kati ya China na Marekani unakuwa tishio kwa uchumi wa dunia.

Katika mkutano wa Paris, unaojikita mwaka huu katika ukuaji wa madeni kwa nchi zinazoendelea, Christine Lagarde, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), ameelezea wasiwasi wake kuhusu mvutano wa biashara unaoendelea kati ya Marekani na China. "ilikuwa inaonekana kama tishio lilikuwa limekwisha, kwamba uhusiano ulikuwa unaenda vizuri, kwamba mkataba unatarajiwa kufikiwa. Tulitarajia kuwa njia hiyo ndio inayofuata, lakini leo, uvumi, kauli mbovu zinakwamisha mkataba huo, " amesema Bi Lagarde.

Azimio la mvutano wa kibiashara kati ya Marekani na China ni "muhimu" kwa kutoathiri ukuaji wa dunia, ameongeza Mkurugenzi Mkuu wa IMF. "Kwa upande mmoja, [ni muhimu] kupunguza au hata kuondoa mvutano, pili kupitishwa kwa mfumo wa kisheria na udhibiti ambao wadau, yaani makampuni yanayohusika katika biashara ya kimataifa, kujua katika mazingira gani, yanayotoza ushuru au la, yanaweza kuendelea kuendeleza shughuli zao. Kuna ulazima kila upand kuondoa dhana mbaya kwa upande mwengine. Hiyo ni sharti ya kwanza. Jambo la pili, bila shaka, ikiwa mvutano unapungua, hii itaruhusu mfululizo mzima wa mazungumzo yanayoendelea, mijadala mingine, hususan kuhusu ushiriki wa nchi kadhaa katika ufadhili wa miundombinu inayohitajika, hasa katika nchi zinazoendelea. "

China na Marekani zatarajia kukutana tena Alhamisi na Ijumaa

Kiongozi wa ujumbe wa China Liu He atasafiri kwenda Washington kwa ziara ya siku mbili, siku ya Alhamisi, Mei 9 na Ijumaa, Wizara ya Biashara ya China imesema Jumanne, licha ya uamuzi wa Donald Trump wa kuongeza ushuru wa dola bilioni 200 kwa bidhaa kutoka China kuinvia nchini Marekani.