Pata taarifa kuu
MAREKANI-CHINA-USHIRIKIANO-UCHUMI

Vita vya biashara kati ya Marekani na China vyaendelea

Rais wa Marekani Donald Trump, Juni 25, 2019.
Rais wa Marekani Donald Trump, Juni 25, 2019. MANDEL NGAN / AFP

Wakati nchi zenye kustawi kiuchumi, G20, zikitarajia kukutana jijini Osaka mnamo Juni 28-29, rais wa Marekani Donald Trump anatarajia kuweka mfululizo wa vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Beijing.

Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivyo vinaweza kuathiri mauzo ya nje ya China kuanzia mwezi Julai. Na kama vikwazo hivyo havitatosha, rais wa Marekani anapanga hatua nyingine inayohusiana na viwango vya ubadilishaji wa sarafu za dunia.

Donald Trump ameagiza Wizara ya Biashara ya Marekani kutayarisha sheria mpya ambayo Marekani inaweza kuwa pekee, yenye uwezo wa kuhukumu ikiwa hatua za sera za fedha zinazochukuliwa mahali pengine duniani zinaathiri maslahi ya Marekani.

Kwa mpango huo, Marekani inaweza kuweka ushuru wa forodha kama adhabu kwa nchi yoyote ambayo wanaamini ingeweza kudhoofisha sarafu yake ili kufanya mauzo yake ya bei nafuu kuliko bidhaa za Marekani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.