Pata taarifa kuu
EU-MAREKANI-BIASHARA-UCHUMI

Vikwazo vya Marekani: Umoja wa Ulaya waapa kulipiza kisasi

Vikwazo hivyo ni sehemu ya vita katika kesi kati ya mashirika mawili ya kutengeneza ndege, Boeing na Airbus.
Vikwazo hivyo ni sehemu ya vita katika kesi kati ya mashirika mawili ya kutengeneza ndege, Boeing na Airbus. REUTERS/Regis Duvignau/File Photo
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Umoja wa Ulaya umeahidi kujibu vikwazo vya Marekani kuhusu bidhaa za Ulaya, huku ukitarajia kufikia makubaliano ya amani na Washington ili kuepukana na vita vya kibiashara.

Matangazo ya kibiashara

"Ikiwa Marekani itachukuwa vikwazo, itakuwa ni shinikizo kwa Umoja wa Ulaya kufanya vivyo hivyo," alionya Daniel Rosario, msemaji wa Tume ya Ulaya Alhamisi wiki hii.

Siku moja kabla, mivutano kati ya Brussels na Washington iliibuka tena ghafla wakati mamlaka nchini Marekani ilitangaza kutaka kutoza kodi bidhaa kutoka Ulaya zenye thamani ya dola bilioni 7.5, baada ya kupewa idhni na Shirika la Biashara Duniani (WTO) kama sehemu ya vita vya miaka 15 katika kesi kati ya mashirika mawili ya kutengeneza ndege, Boeing na Airbus.

Kulingana na hukumu ya kesi iliyotolewa na Shirika la Biashara Ulimwenguni, WTO, Marekani inaweza kuziwekea ushuru bidhaa za Ulaya ili kulipiza kisasi ruzuku hizo kwa Airbus ambazo zimekuwa na athari kwa mpinzani wake nchini humo, Boeing.

Alhamisi asubuhi hii, Rais wa Marekani, Donald Trump alikaribisha uamuzi wa WTO, akipongeza "ushindi mkubwa". Washington imesema hatua ya ongezeko hili la tozo kwa bidhaa hizo itaanza kutekelezwa Oktoba 18.

Marekani imesema inajiandaa kuziwekea ushuru bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 7.5 zinazotoka Umoja wa Ulaya, ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi ruzuku isiyo halali ya umoja huo kwa kampuni inayotengeneza ndege ya Airbus.

Kulingana na ofisi ya mwakilishi wa biashara wa Marekani, nchi hiyo inapanga kuweka ushuru wa asilimia 10 kwenye ndege zinazoingizwa kutoka Ulaya na asilimia 25 ya kodi za bidhaa za kilimo na viwanda zinazoingizwa nchini humo ifikapo Oktoba 18. WTO ilipitisha kiwango cha ruzuku kwa asilimia 100, lakini Marekani iliamua kuweka ukomo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.