CHINA-MAREKANI-BIASHARA-UCHUMI

Huawei kuhamisha maabara yake ya utafiti kutoka Marekani kwenda Canada

Kituo cha utafiti cha Huawei California, Futurewei, tayari kimepunguza wafanyakazi wake 250, kwa sababu ya vikwazo vilivyowekwa na serikali ya Marekani.
Kituo cha utafiti cha Huawei California, Futurewei, tayari kimepunguza wafanyakazi wake 250, kwa sababu ya vikwazo vilivyowekwa na serikali ya Marekani. REUTERS/Aly Song

Kiongozi Mkuu wa kampuni ya simu ya Huawei, Ren Zhengfei, ametoa tangazo katika mahojiano na The Globe and Mail, Gazeti kubwa la kila siku Canada kwamba maabara ya utafiti ya Huawei yatahamishwa kutoka Marekani kwenda Canada.

Matangazo ya kibiashara

Uhusiano kati yaChina na Canada umekuwa mbaya kwa mwaka mmoja sasa, tarehe ambayo binti wa kiongozi mkuu wa Huawei alikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Vancouver.

Hii ni sura nyingine mpya ya vita ya biashara kati ya China na Marekani. Baada ya kukasirishwa na kutokuepo na mawasiliano kati ya kampuni yake na wafanyakazi wake waishio California huko katika eneo la Silicon Valley, tangu Marekani kuchukuwa hatua za dhidi ya kamuni ya Huawei, kiongozi mkuu wa kampuni hiyo ameamua kuchukuwa hatua za kujibu. Ren Zhengfei atahamisha wafanyakazi wake na maabara ya utafiti ya Huawei kaskazini mwa Canada, amesema katika mahojiano yaliyochapishwa na gazeti la Canada la Globe and Mail.

Kwa mujibu wa Ren Zhengfei, kampuni ya China ya Huawei, iliyobobea kwa simu mahiri za Smartphones na mitandao ya mawasiliano inayotumiwa bila waya itaanza kusambaza ofisi zake nchini Canada.

Hivi karibuni utawala wa Washington uliiorodhesha Huawei katika msururu wa makampuni ambayo Marekani imeyapiga marufuku kufanya nao biashara labda tu wapate leseni maalumu.

Makataa haya ya kibiashara ni sehemu ya vita ya kibiashara baina ya mataifa hayo mawili yenye nguvu duniani..

Marekani ilichukua uamuzi wa kuizuia Huawei ambayo ni wazalishaji wakubwa duniani wa vifaa vya mawasiliano kwa kile ilichodai kuwa kampuni hiyo imekuwa ikidukua taarifa na ni hatari kwa usalama.

Huawei mara zote imekuwa ikikanusha tuhuma za Marekani ikisisitiza kuwa ni kampuni huru na haina uhusiano wowote na Serikali.

Soma zaidi: Mabilioni ya wateja wa Huawei kuathirika na hatua ya Marekani