DRC-ELIMU-UFISADI-UCHUMI

Mvutano waibuka kuhusu udanganyifu mkubwa kwa shule hewa DRC

Udanganyifu huo hauhusu tu waalimu hewa lakini pia shule za zisizokuepo (picha ya kumbukumbu)
Udanganyifu huo hauhusu tu waalimu hewa lakini pia shule za zisizokuepo (picha ya kumbukumbu) RFI/Léa-Lisa Westerhoff

Tuhuma mpya za udanganyifu zimeendelea kuikumba sekta ya elimu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Karibu kila mwaka, mamia ya waalimu hewa wanagunduliwa na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mbunge mmoja kutoka chama cha rais cha UDPS, kasumba hiyo sasa imekuwa kubwa. Hali hiyo haihusu tu waalimu lakini pia shule, zinazosaidiwa na serikali kwa mwaka huu wa kwanza wa elimu ya bure, ikiwa ni kipaumbele cha rais Félix Tshisekedi.

Tony Mwaba, mbunge kutoka chama cha rais Felix Tshisekedi cha UDPS, anasema ana faili za kuthibitisha madai yake. Anadai amepata faili hizo kutoka kwa baadhi ya maafisa serikalini na hata kwa washirika wa serikali. Tony Mwaba amebaini kwamba shule hewa " zinakadiriwa kufikia 2,000 nchini kote. Ameongeza kwamba hali hiyo inawezeshwa na idara inayosimamia Malipo ya Walimu (SECOPE).

"Faili hizo zinajumuisha majina ya watu ambao hawapo lakini pia wafuasi wa vyama vya siasa au watu ambao taaluma yao haina uhusiano wowote na elimu" , amesema mbunge Tony Mwaba.

Akihojiwa, Waziri wa Elimu, Willy Bakonga, ametambua kuwa kitendo hicho kinaweza kuwepo.

Waziri Willy Bakonga amesema kwamba kuna mmoja katika maafisa wa serikali aliweza kupitisha uamuzi wa kuundwa kwa shule hewa 80.

Waziri Bakonga amebaini kwamba uchunguzi umeanzishwa, na matokeo yake yatathibitishwa na ukaguzi wa Benki Kuu ya Dunia.

Mbunge Tony Mwaba, amesema kuwa suala hilo sio tu kwa suala la ufisadi. Amekumbusha kwamba shule hewa pia zinaweza kutumika kama vituo vya kupigia kura na hivyo kuwezesha wizi wa kura wakati wa uchaguzi.