OPEC-MAREKANI-ULAYA-UCHUMI

Bei ya mafuta kutoka Marekani yashuka katika masoko ya Asia

Makao makuu ya OPEC huko Vienna, Austria.
Makao makuu ya OPEC huko Vienna, Austria. REUTERS/Leonhard Foeger

Bei ya mafuta ghafi katika masoko ya Asia imeshuka hadi kufikia dola 15 kwa pipa, kiwango kikubwa ambacho hakijawahi kuonekana kwa zaidi ya miongo miwili.

Matangazo ya kibiashara

Pipa la mafuta kutoka Marekani, West Texas Intermediate (WTI) ambazo zingelitolewa mwezi Mei, zimeshuka bei kwa asilimia 19.27 hadi kufikia dola 14,45 kwa kila pipa, sawa na kiwango chake cha chini kabisa tangu mwaka 1999, shirika la habari la AFP limeripoti. Kwa upande wake, pipa za Brent North Sea, alama ya Ulaya, halijaathiriwa sana, ikitoka asilimia 2,53, hadi kufikia dola 27.37 kwa pipa.

Hali hii inatokea wakati wafanyabiashara wanazidi kuingiwa na wasiwasi kwamba hifadhi zao zinaelekea kufikia kikomo.

Hivi karibuni chi zinazozalisha mafuta ikiwemo Urusi zilikubaliana kupunguza uzalishaji wa bidhaa hiyo kwa asililia kumi ili kukabiliana na bei ambazo zimeyumba kutokana na athari za Corona.

Rais wa Marekani alitoa shinikizo kwa mataifa hayo kutaka bei za mafuta kutathminiwa upya.

Kudorora kwa uchumi, hali iliyo sababishwa na janga la Covid-19 kumesababisha bei ya mafuta kushuka kwa kiwango cha chini kabisa. Bei ya mafuta imeshuka kwa zaidi ya 50% tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Baada ya siku kadhaa za mazungumzo na mikutano kadhaa ambayo haikuzaa matunda yoyote, hatimaye OPEC, Jumuiya ya nchi zinazozalisha mafuta duniani na washirika wake walifikia makubaliano ya kupunguza kiwango cha uzalishaji kwa karibu mapipa milioni 10 kwa siku kuanzia mwezi Mei, waziri wa Mexico aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter.