MAREKANI-CHINA-BIASHARA-UCHUMI

Washington na Beijing zadumisha mkataba wao wa biashara

Katika mazungumzo ya simu Mei 8, 2020, China na Marekani zilikubaliana kuandaa mazingira mazuri kwenye mkataba awamu ya 1 uliyotiliwa saini Januari 2020.
Katika mazungumzo ya simu Mei 8, 2020, China na Marekani zilikubaliana kuandaa mazingira mazuri kwenye mkataba awamu ya 1 uliyotiliwa saini Januari 2020. Greg Baker / AFP

Wadau wakuu katika mazungumzo kuhusu biashara kutoka China na Marekani wamefanya mazungumzo yao ya kwanza kwa simu leo Ijumaa Mei 8 tangu kuanza kwa janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe kutoka nchi hizo mbili wamekubaliana kufanya kazi kwa pamoja kuwezesha utekelezaji wa mkaba wa biashara ya "awamu ya 1" uliyotiliwa saini mwezi Januari kati ya nchi hizi mbili zenye uchumi mkubwa duniani.

Wengi wanajiuliza iwapo vita vya kibiashara kati ya China na Marekani vinaweza tena kutokea.

Katika taarifa iliyotolewa na shirika la habari la serikali ya China la Xinhua, Wizara ya Biashara ya China imesema kwamba Naibu Waziri Mkuu wa China Liu He, mwakilishi wa biashara wa Marekani, Robert Lighthizer, na Waziri wa Fedha wa Marekani Steven Mnuchin, wamekubaliana kwamba China na Marekani zitafanya kazi kwa pamoja kuandaa mazingira mazuri ya utekelezaji wa mkataba wa biashara ya "awamu ya 1" uliyotiliwa saini mnamo mwezi Januari mwaka huu.

Pande zote mbili zimesema kuna "maendeleo" ambayo yamefikiwa ili kuheshimu masharti ya mkataba huo, ofisi ya Robert Lightsizer imebaini katika taarifa tofauti.

Ofisi yake imesema kuwa Washington na Beijing wanatarajia kutimiza ahadi zao licha ya mgogoro wa kiafya uliyopo. Maafisa wa Marekani na China wataendelea kufanya mikutano ya kawaida kupitia video, ofisi ya Lightsizer imeongeza.