MAREKANI-CORONA-UCHUMI

Corona yasababisha uchumi wa Marekani kushuka kwa asilimia 32.9

Mwezi Aprili pekee, zaidi ya ajira Milioni 20 zilipotea nchini Marekani, baada ya biashara kufunga na watu kusalia nyumbani kutokana na janga la Corona.
Mwezi Aprili pekee, zaidi ya ajira Milioni 20 zilipotea nchini Marekani, baada ya biashara kufunga na watu kusalia nyumbani kutokana na janga la Corona. REUTERS/Mike Segar

Uchumi wa Marekani umeshuka kwa asilimia 32.9 kutokana na janga la Corona, iikiwa ni pigo kwa rais Donald Trump kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba.

Matangazo ya kibiashara

Kushuka kwa uchumi nchini Marekani kumeshuhudiwa kati ya mwezi Aprili na Juni, kwa mujibu wa watalaam wa masuala ya uchumi, katika kipindi ambacho nchi hiyo imekuwa ikishuhudiwa idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Mwezi Aprili pekee, zaidi ya ajira Milioni 20 zilipotea nchini humo, baada ya biashara kufunga na watu kusalia nyumbani kutokana na janga la Corona.

Wiki iliyopita pekee, watu Milioni Moja na Laki nne waliripoti kupoteza ajira katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa duniani, wakati huu wachambuzi wakibashiri kuwa hali huenda ikawa mbaya zaidi katika siku zijazo kabla ya uchumi kuanza tena kuimarika taratibu.

Wanasaisa wa chama cha Republican na Democratic, wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusu namna ya kuimarisha tena uchumi wa taifa hilo kutokana na janga la Coroana wakati huu taifa hilo likielelea kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Nevemba.