WTO-DUNIA-UCHAGUZI

Uchaguzi wa kiongozi mpya wa WTO: Wanawake watatu waingia mzunguko wa pili

Balozi wa Amina Mohamed, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Kenya, ni miongoni mwa wanawake watatu wamefanikiwa kufika katika mzunguko wa pili katika harakati za kumsaka kiongozi mpya wa Shirika la Biashara duniani.
Balozi wa Amina Mohamed, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Kenya, ni miongoni mwa wanawake watatu wamefanikiwa kufika katika mzunguko wa pili katika harakati za kumsaka kiongozi mpya wa Shirika la Biashara duniani. UN Photo/JC McIlwaine

Wanawake watatu, wakiwemo wawili kutoka barani Afrika na mmoja kutoka Korea Kusini, wamefanikiwa kufika katika mzunguko wa pili katika harakati za kumsaka kiongozi mpya wa Shirika la Biashara duniani.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti za Kidiplomasia kutoka Geneva zinaeleza kuwa, wanawake hao ni Amina Mohamed kutoka nchini Kenya, Ngozi Okonjo-Iweala kutoka Nigeria na Yoo Myung-hee kutoka Korea Kusini.

Hakuna mwanamke au Mwafrika amewahi kuongoza Shirika hilo, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1995.

Pamoja na wanawake hao watatu, kuna wanaume wawili ambao pia wapo kwenye kinyanganyiro hicho cha kuchukua nafasi ya Roberto Azevedo, ambaye ajiuzulu mwaka uliopita.

Wanaume wawili ambao wamesalia katika orodha hiyo kupambana na wanawake hao ni pamoja na Liam Fox kutoka Uingereza na Mohammed Al-Tuwaijri kutoka Saudi Arabia.

Kumekuwa na wito wa nafasi hiyo kumwendea Mwafrika, kuongoza Shirika hilo kubwa la biashara duniani.

Nchi wananchama wa WTO wapatao 164, wanatarajiwa kufanya uamuzi wa kiongozi mpya ifikapo mapema mwezi Novemba, huku mchakato wa Uchaguzi ukifanyika kati ya Septemba tarehe 24 hadi Oktoba 6.