Kwa picha: siku ya kwanza ya Rais Macron baada ya kukabhidiwa madaraka

Rais mteule wa Ufaransa akikagua majeshi yake katika bustani ya ikulu ya Elysées, Mei 14, 2017. REUTERS/Gonzalo Fuentes

Emmanuel Macron. Jumapili hii, amekua rasmi rais wa Ufaransa akiwa na umri wa miaka 39. Emmanuel Macron ni rais wa nane wa awamu ya 5 wa Jamhuri ya Ufaransa. Rais Emmanuel Macron alikabidhiwa madaraka na mtangulizi wake François Hollande siku ya Jumapili Mei 14. Baada ya sherehe ya kukabidhiwa madaraka ya uongozi wa nchi, Emmanuel Macron alizuru eneo la Arc de Triomphe kuwasha mwenge katika kumbukumbu ya askari waliofariki wakiwa kazini. Nae Mkuu mpya wa majeshi alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya kijeshi ya Percy mjini Clamart.

Matangazo ya kibiashara