SHOW-TANZANIA_SMADJ

RFI Talent inawaletea msanii Smadj Tanzania!

Jean-Pierre Smadja, almaarufu Smadja.
Jean-Pierre Smadja, almaarufu Smadja. © RFI

Pata uhondo wa msanii mashuhuri katika tamasha kabambe kwenye ukumbi wa Alliances Françaises,Mei 20 Arusha, Mei 21 Zanzibar na Mei 24 Dar es Salaam.

Matangazo ya kibiashara

Jean-Pierre Smadja, almaarufu Smadja, alizaliwa nchini Tunisia, na alikua mara nyingi akisikiliza muziki wa Mashariki, Funk na Soul, muziki wa Brazil na muziki wa kitamaduni.

Baada ya albamu ya kwanza iliyotolewa mwaka 1994, inayojulikana kwa jina la "Tatoom presente Tatoom", ambayo ilitambulika katika ukumbi wa kimataifa mwaka 2000 pamoja na albamu inayojulikana kwa jina la Equilibriste, iliyovunja rekodi na ambayo imejizolea sifa tele ulimwenguni. Kwa sasa inachukua nafasi ya nne katika ulimwengu wa muziki Ulaya.

Muziki aina ya Charts & quot; unaochezwa kwa miaka kumi na tano sasa, msanii huyu shupavu ameweza kurekodi albamu nyingi na watu muhimu kimataifa kama vile Mehdi Haddab, Talvin Singh, Rokia Traoré, Erik Truffaz, Natacha Atlas ... Pamoja na albamu yake ya hivi karibuni "Spleen" (RFI Talent / Jazz Village), Smadj anaendelea kujizolea sifa katika nchi mbalimbali duniani. Kwa sasa ameanzisha mradi mwengine unaojulikana kama "OudSolotronic". Daniel Lieuze

Taarifa zaidi tembelea tovuti hii:

http://www.smadjmusic.com/

Mei 21 Arusha, Mei 21 Zanzibar na Mei 24 Dar Es Salaam kwenye ukumbi Alliances Françaises.