UHISPANIA

Maharamia wahukumiwa kifungo jela nchini Uhispania

Bendera ya Uhispania
Bendera ya Uhispania

Mahakama moja nchini Uhispani imewahukumu kifo cha miaka mia nne na thelathini na tisa Maharamia Wawili wa Kisomalia ambao wamewakuta na hatua ya kuteka meli yao ya uvuvi ikiwa na wafanyakazi wake mwezi Oktoba mwaka elfu mbili na kenda.

Matangazo ya kibiashara

Maharamia hao Abdou Willy na Raagegeesey Adji Hamanwere walikamatwa siku mbili baada ya kuiteka meli hiyo na kisha kupelekwa nchini Uhispani kufunguliwa mashtaka yao ya utekaji nyara.

Maharamia hao wamekutwa na hatia ya kutenda makosa thelathini na sita kila mmoja ikiwemo ugaidi na wizi wa kutumia silaha na tayari Mahakama imewaamuru kulipa Euro laki moja kila mmoja.