UTURUKI

Maofisa wanne wajeruhiwa wakati wa maandamano ya Kikurdi

Maofisa wa serikali nchini Uturuki wamejeruhiwa katika maadnamano yalioshuhudiwa nchini humo.

Waandamanaji wa Kikurdi wakipambana na Polisi
Waandamanaji wa Kikurdi wakipambana na Polisi REUTERS/Osman Orsal
Matangazo ya kibiashara

Umati wa Waandamanji wa Kikurdi wameshambulia gari la polisi Kusini Mashariki mwa Uturuki nakusababisha maofisa wanne kujeruhiwa katika tukio linalotajwa ni la kulipiza kisasi baada ya kifo cha waasi wanne.

Umati huo wa Waandamanji ambao ulikuwa unatoka kwenye mazishi ya Wakurdi hao wanne ambao waliuawa kwenye mapambano na Jeshi uliamua kufanya mashambulizi katika Jiji la Diyarbakir ambapo kuna Wakurdi wengi.

Watu hao wakiwa wanaimba wimbo ya kulipiza kisasi kulipiza kisasi huku wakiwa na bendera za Kukurdi ambacho kimegawanyika cha PKK wamejiapiza kuhakikisha damu uliyomwagika inalipwa.