UHISPANIA

Tetemeko la ardhi latikisa Jiji la Kihistoria nchini Uhispania

Wanajeshi na Wafanyakazi wa Mashirika la Kutoa Misaada wamesimama imara katika kuweka mahema kuwasaidia maelfu ya wananchi nchini Uhispania ambao wamehamishwa baada ya nchi hiyo kupigwa na tetemeko lenye kipimo cha 5.1.

Jiji la Kihistoria la Lorca nchini Uhispania likiwa limepigwa na tetemeko la ardhi
Jiji la Kihistoria la Lorca nchini Uhispania likiwa limepigwa na tetemeko la ardhi REUTERS/Francisco Bonilla
Matangazo ya kibiashara

Tetemeko hilo ambalo limepiga Jiji la Kihistoria nchini Uhispani limesababisha vifo vya watu wanane akiwemo mtoto mdogo na wengine 130 wakijeruhiwa Kusini Mashariki mwa Lorca.

Tetemeko hili ni kubwa zaidi kuwahi kutokea katika nchi hiyo katika kipindi cha miaka 50 serikali ya mkoa imethibitisha pamoja na kutaja madhara ambayo yamechangiwa na tukio hilo.

Mkuu wa Masuala ya Dharura katika Mkoa huo Luis Gestoso amekiri majengo kadhaa kuthiriwa huku nyumba nyingi zikipata nyufa hali ambayo imechangia majeruhiwa kuwa wengi.

Serikali tayari imeshawahamisha wakazi 93,000 ambao walikuwa wanaishi kwenye Jiji hilo la Kihistoria ili kuwaepusha na madhara zaidi ambayo yanaweza kutokea.

Majengo zaidi ya 20,000 ambayo mengi yalitengenezwa kwenye karne ya 16 na 17 yaliharibiwa na tetemeko hilo katika Jiji la Lorca yakiwa na umei wa zaidi ya miaka 2000.

Meya wa Lorca Francisco Jodar amethibitisha asilimi 80 ya majengo ya Jiji lake yameharibiwa na tetemeko hilo huku mnara wa saa uliokuwa kwenye Kanisa la San Diego ikiharibiwa kabisa.

Meya Jodar amesema hakuna mtu ambaye alithubutu kulala nyumbani kwake usiku wa kumkia alhamisi wakati Jiji la Lorca likishuhudia tetemeko hilo baya katika kipindi cha miaka 50.

Tayari serikali imetuwa watu 800 nusu yao wakiwa wanajeshi lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi kupata makazi wakati huu ambapo juhudi za kuwapa msaada zaidi zinafanywa.