ziara

Kifurushi cha bomu cha gunduliwa muda mchache kabla ya ziara ya Malkia Elizabeth II nchini Ireland

ziara ya Malkia'Elisabeth II
ziara ya Malkia'Elisabeth II REUTERS/Phil Noble

Bomu lagunduliwa mjini Dublin Jamuhuri ya Ireland muda mchache kabla ya ziara ya Malkia Elisabeth II nchini Ireland. Jeshi la nchi hiyo limetangaza kulipua bomu hilo la ambalo lilikutwa katika kifurushi ndani basi la usafiri wa abiria.

Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya Ireland ya mambo ya kigeni imetangaza kwamba ziara ya malkia huyo nchini Irland itafanyika kama ilivyopangwa.
Vyombo vya usalama vimezidisha ulinzi na kuwekwa katika hali ya taharuki kudhibiti usalama wa Malkia Elizabeth ambae anafanya ziara hiyo ya kwanza kabisa kufanywa na mtu wa familia ya kifalme nchini Ireland tangu mfalme Georges V mwaka 1911.

Bomu hilo liligunduliwa katika mji wa Maynooth ulioko kwenye umbali wa kilometa 25 na mji wa Dublin. Jeshi liliwatuma wataalamu wake katika vitongoji mbalimbali vya mji huo kama ilivyo ombwa na polisi. Mabaki ya bomu hilo yalikabidhiwa polisi kwa uchunguzi zaidi.