MAREKANI-UFARANSA

Mkurugenzi wa IMF Dominique Strauss-Kahn, anyimwa dhamana

Dominique Strauss-Kahn akionekana mchovu mbele ya mahakama ya uhalifu ya  Manhattan, Mei 16, 2011.
Dominique Strauss-Kahn akionekana mchovu mbele ya mahakama ya uhalifu ya Manhattan, Mei 16, 2011. REUTERS/Andrew Gombert/Pool

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la fedha duniani IMF, Dominique Strauss-Kahn anazuiliwa kizuizini jijini New York Marekani, baada ya kufunguliwa mashtaka ya tuhuma ya ubakaji dhidi ya muhudumu wa hoteli aliyokuwa anaishi huko New York juma lililopita.

Matangazo ya kibiashara

Jaji Melissa Jackson aliyesikiliza mashtaka hayo, alikataa kumuachilia Strauss-Kahn kwa dhamana ya milioni moja dolari za kimarekani kama walivyopendekeza mawakili wake, na kuweka kibali chake cha usafiri kwenye mahakama hiyo na kusalia jijini New York kwa binti yake katika kipindi hiki kesi ikiendelea kusikilizwa. Licha ya mapendekezo yote hayo jaji Melisa Jackson aliamuru kiongozi huyo asalie kiziuzini. Ikiwa itathibitishwa alitekeleza ubakaji atafungwa jela miaka ishirini na mitano.

Mmoja kati ya mawakili wake Benjamin Brafman amesema inasikitisha kuwa mahakama ya New York imekataa kumuacha huru mteja wake kwa dhamana, na kuongeza kuwa ndio mapambano yameamza na anaamini kuwa mteja wake hana makosa yeyote na atashinda kesi hiyo. Awali habari zilitanda ulimwenguni kuwa DSK alijaribu kukimbia. Wakili huyo alikanusha habari hizo na kusema kwamba muda huo DSK alikuwa amekwenda kupata lishe akiwa na binti yake ambae anaedshi New York marekani.

Jopo la majaji 23 watakutana siku ya Ijumaa na watakagua shutuma dhidi ya DSK iwapo zinatosha kufunguliwa mashtaka  ao la. Vinginevyo jopo hilo la majaji laweza kuamuru kuachuliwa huru kwa kiongozi huyo wa IMF. Hata hivyo wakaguzi wa mambo wanasema kuna uwezekano mdogo wa kuamuru achiwe huru.