London, Uingereza

Obama azungumzia usalama wa dunia akiwa Uingereza

RFI

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa ushirikiano baina ya nchi yake na Uingereza ni muhimu katika kujenga uhusiano mwema na unapaswa kuendelezwa.

Matangazo ya kibiashara

Rais Obama ametoa kauli hiyo akiwa katika ziara yake ya siku tatu nchini Uingereza na amekutana na Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza katika kasri la kifalme nchini humo.

Obama amesema kuwa endapo Uingereza na Marekani zitasimama pamoja katika ushirikiano basi watu wengi duniani watakuwa salama na kupata mafanikio zaidi.

Jumatano wiki hii Obama atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ikiwa ni sehemu ya ziara hiyo.

Katika mkutano huo hoja zinazotarajiwa kuzungumziwa ni pamoja na hali ya kisiasa na usalama katika eneo la mashariki ya kati na mgogoro wa Libya.