Uhispania, Ujerumani

Chanzo cha maradhi ya kuharisha hakikutokea nchini Uhispania

Matango kutoka Uhespania yauzwa mjini Berlin nchini Ujerumani Mei 27, 2011.
Matango kutoka Uhespania yauzwa mjini Berlin nchini Ujerumani Mei 27, 2011. REUTERS/Tobias Schwarz

Serikali ya Hispania inapania kuchukuwa hatua za kisheria dhidi ya mamlaka ya Hamburg kwa ajili ya kutangaza kwamba matango kutoka Uhispania kuwa chanzo cha kuzuka kwa maradhi hatari ya kuharisha huko kaskazini mwa Ujerumani.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka za afya katika mji wa Hamburg wamekubali Jumanne kwamba vipimo vinaonyesha kuwa chanzo hasa cha maradhi hayo hakikutoka Uhispania

Akizungumza kwenye radio Cadena ser, waziri wa mambo ya ndani wa Uhespania Alfredo Perez Rubalcaba amesema “chanzo cha maradhi hayo hakikutokea Uhispania”

"Mara baada ya ukweli kugundulika , inabakia kukarabati mazingira yaliotokana na kutowa habari zisizo sahihi, na hilo ni muhimu,"aliongeza.

Wazalishaji wa matunda na mboga wa Uhispania wanapiga kelele jumanne kutokana na kupungua kwa mauzo juu habari hiyo isiyo sahihi iliozagaa katika nchi za umoja wa ulaya kuhusu matunda ya uhispania kusababisha virusi vya maradhi ya kuharisha.

Shirikisho la Kihispania ya Wazalishaji na wauzaji wa matunda na mboga mboga (FEPEX) imetowa tathmini ya hasara inayo fikia " euro milioni 200 kwa wiki."

"Hatuwezi kuweka kando uwezekano wa kufungua mashtaka dhidi ya viongozi walioshukia bidhaa zetu .Tunaweza kuchukua hatua katika kesi hii, dhidi ya mamlaka ya Hamburg., " alisema Rubalcaba.

Waziri wa Kilimo Rosa Aguilar aliuliza Jumanne katika mkutano na wenzake wa Ulaya nchini Hungary "kuhusu hatua ya kutowa msaada wa dharura kwa wakulima, " ilithibitisha taarifa kutoka mamlaka ya wizara hiyo.

Uchambuzi juu ya matango na udongo zilizokusanywa kutoka kwa wazalishaji wawili wa Andalusia (kusini) wanaohusishwa nchini Ujerumani, wafanyika kwa sasa maabara ya Hispania.