BRUSSELS-MAREKANI

Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates aishutumu NATO

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates akihutubia
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates akihutubia REUTERS

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates ambaye anamaliza muda wake ifikapo mwishoni mwa mwezi huu ameushutumu vikali Umoja wa nchi za magharibi za kujihami NATO kuhusiana na operesheni inazozifanya nchini Libya.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mjini Brussels wakati akihutubia mkutano wake wa mwisho akiwa kama waziri wa ulinzi wa Marekani, Gates amesema kuwa katika historia ya vikosi hivyo hajawahi kuona operesheni mbaya ambayo haijajipanga inayofanywa nchini Libya.

Amesema kuwa ni wiki kumi na moja sasa tangu vikosi vya NATO vimeanzisha operesheni dhidi ya vikosi vya Moamer Gaddafi lakini vikosi hivyo vimeshuhudiwa vikishindwa kufanya kazi zake ipasavyo na kushuhudia majeshi ya Kanali yakiwazidi uwezo katika kufanya mashambulizi.

Waziri huyo ameongeza kuwa opereresheni ya vikosi hivyo inaonekana kushindwa kufanya kazi vizuri nchini Libya kutokana kukosekana kwa umoja toka nchi wanachama wa umoja huo ambao hawajashiriki moja kwa moja kutoa mchango wa wanajeshi katika kutekeleza operseheni.

Waziri Gates amesema kuwa chakusikitisha katika operesehni ya safari hii ni kuwa wanachama wachaceh zaidi wameonekana kuwa mstari wa mbele kutoa vikosi vyake kushirikiana katika operesehni nchini Libya hali inayokwamisha juhudi za kuifanya iwe ya mafanikio nchini humo.

Kiongozi huyo amemaliza kwakusema kuwa ili operesheni ya kijeshi nchini Libya iweze kufanikiwa, ni lazima kipatikane kiasi cha fedha cha zaidi ya dola za marekani Bilioni 300 na kusema kuwa opersehni ya sasa imepatikana chini ya hapo.

Amezitaka nchi za Hispania, uturuki, na uholanzi kuongeza nguvu zaidi atika vikosi vya NATO nchini Libya hasa kwa kupeleka ndege za kivita za kushambulia ili kurahisisha operesheni hiyo.