ITALIA-Berlusconi

Serikali ya waziri mkuu wa Italia yaponea chupuchupu

Waziri mkuu wa Italia Silvio Berlusconi,
Waziri mkuu wa Italia Silvio Berlusconi, REUTERS/Stephane Mahe

Serikali ya Italia inayoongozwa na waziri mkuu Silvio Berlusconi imefanikiwa kushinda kikwazo cha kupigiwa kura ya kutokuwa na imani nayo wakati ikiwasilisha muswada wa masuala ya uchumi, hatua inayokuja baada ya kufanya vibaya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Matangazo ya kibiashara

Kura hiyo ilikuwa inapigwa wakati wa kupitishwa kwa mswada wa sheria ya kufanyika kwa mabadiliko ya uchumi huku serikali hiyo ikitangaza mpango wake wa kupunguza baadhi ya kodi.

Serikali ya Waziri Mkuu Berlusconi imeshinda kura hiyo kwa kupata alama mia tatu na kumi na saba dhidi ya mia mbili na tisini na tatu ambazo ziliipinga huku wabunge wawili pekee wakikosekana wakati zoezi hilo linafanyika.