Urusi-Ajali

Watu 44 wauawa katika ajali ya ndege nchini Urusi

Petrozavodsk, Juni 21, 2011. ndege Tupolev ya kampuni ya RussAir ilioanguka muda mchache kabla ya kutua
Petrozavodsk, Juni 21, 2011. ndege Tupolev ya kampuni ya RussAir ilioanguka muda mchache kabla ya kutua © Reuters/Vladimir Larionov

Watu arobaini na wanne wamepoteza maisha papo hapo, na wengine nane kupata majeraha, baada ya ndege kuanguka barabarani, na kuwaka moto, huko kaskazini mwa Urusi. Ndege hiyo iliokuwa na jumla ya abiria 52 ilianguka na kukatika vipande. Miongozi mwa manusura yumo kijana mdogo mwenye umri wa miaka 9 na dada yake.

Matangazo ya kibiashara

Kutokana na hali mbaya ya hewa, rubani wa ndege hiyo The RussAir Tu-134, alikuwa akijaribu kutua kwa dharura, dakika chache tu, kabla ya saa sita usiku wa kuamkia leo, umbali wa kilomita mbili hivi kutoka uwanja wa ndege wa Petrozavodsk, mkoa wa Karelia, mwisho wa safari yake.

Uchunguzi umeanzishwa kutaka kujuwa kiini cha ndege hiyo kujaribu kutuwa kwa dharura barabarani muda mchache kabla ya kufika kwenye uwanja wa ndege uliosalia kwenye umbali wa kilometa mia saba.

Wachunguzi wa urusi wanaangalia iwapo ajali hiyo ilitokana na kosa la kiutu, hali ya hewa ao matatizo ya kiufundi. hali ya ndege hiyo itachunguzwa pia. Ndege hiyo nusra iangukie majumba ya raia. Ilivunjika vipande viwili na kuteketea kwa moto.