France

Martine Aubrey ajitangaza kuwa mgombea kiti cha urais nchini Ufaransa mwaka 2012

A dirigente do Partido Socialista francês, Martine Aubry, em conferência em Lille nesta terça-feira (28).
A dirigente do Partido Socialista francês, Martine Aubry, em conferência em Lille nesta terça-feira (28). Reuters

“Nimeamuwa kujipendekeza kuwa mgombea kwenye kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka 2012” hivyo ndivyo alivyo tamka Martine Aubry katibu mkuu wa chama cha Socialist PS wakati akitangaza jumanne Juni 28 kuwa mgombea katika uchaguzi wa awali ambao unaashiria kuwania kiti cha uraia katika uchaguzi unapangwa kufanyika kwaka 2012. uchaguzi wa wali umepangwa kufanyika Octoba 9 na 16 mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Mwanamama huyo wengi walimchukulia kama mwenye kusitasita, huku wengine wakimzungumzi akutokuwa na nia y kuwania urais. Binti wa Jacques Delors aliejiondowa kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 1995, sasa ajitowa kugombea kiti hicho na kusema kuwa” Nimeamuwa kuwa mgombea wa kiti cha urais”

Martin Aubrey ametangaza hatuwa hiyo akiwa katika makao makuu ya chama hicho mjini lille. Ktibu mkuu wa chama cha Socialist ambae anapewa kipao mbele pamoja na Francois Hollande aliwantangazia wafaransa wakati wa uzinduzi wa kujiorodhesha kuwania kiti hicho katika uchaguzi wa mwanzo wa Octoba ijayo ambapo chama hicho kitawakilisha mgombea kwenye kiti cha urais wa mwaka 2012