Ugiriki

Vyama vya wafanyakazi nchini Ugiriki vyagoma saa 48

Polisi ya zima moto ikitekeleza jukumu lake
Polisi ya zima moto ikitekeleza jukumu lake REUTERS/Yannis Behrakis

Mgomo wa saa 48 umeanza nchini ugiriki ,wakati bunge la nchi hiyo likitarajiwa kupiga kura muhimu juu ya kupitisha ama kutopitisha mpango wa serikali ya nchi hiyo kubana matumizi  

Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya waandamanaji wamekusanyika nje ya jengo la bunge mjini Athens huku huduma za usafiri wa uma zikisimama nchini humo pamoja na huduma nyingine za Afya,benki,na huduma za usafiri wa anga.na baadae kutokea hali ya purukushani baada ya makundi madogo madogo ya waandamanaji kupigana na vikosi vya usalama vya nchini humo ambao nao walitumia gesi za machozi kuwatawanya.

Gadhabu hiyo imekuja huku vyama vya wafanyakazi vikisema mpango wa kubana matumizi utawaathiri raia wenye kipato kidogo kwa kuwaongezea kodi baada ya miezi kadhaa ya kubana matumizi ya serikali na kufanya kukosekana kwa ajira kwa kiasi cha zaidi ya asilimia 16.

Waziri mkuu wa nchi hiyo,George Papandreou amesema kiasi cha euro bilioni 28 zinahitajika kukatwa kupunguzwa kutoka kwenye bajeti ya matumizi ya serikali na ikiwa itashindwa kufanya hivyo umoja wa ulaya EU na Benki ya dunia IMF haitapata mkopo wa euro bilioni 12 na hivyo kuifanya ugiriki kufilisika.

Hapo jana Papandreou aliwaomba wabunge nchini humo kuunga mkono hatua ya kupunguza matumizi kwa kukata kiasi cha euro bilioni 26.8 kwa mwaka 2015 ili kuweza kutimiza masharti ya EU na IMF.

Mkuu wa maswala ya uchumi kutoka umoja wa ulaya, Olli Rehn,amelitaka bunge la ugiriki kuukubali mpango huo ili kuepuka hasara.

Wabunge nchini humo wanatarajiwa kupiga kura hapo kesho kuidhinisha mpango huo.